LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA ATANGAZA KIAMA KWA MACHINGA WASIOTII SHERIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza jana katika eneo la Msikiti wa Temple Makoroboi wakati wa zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) katika eneo hilo ambalo si rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
Na BMGKiomoni alisema machinga hawaruhusiwi na hatawaruhusiwa kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi Jijini Mwanza ikiwemo eneo hilo ambalo huduma za kijamii ikiwemo dini na shule zinapatikana.

Alisema hakuna upungufu wa maeneo ya machinga kufanyia biashara hivyo wale walio katika maeneo yasiyo rasmi katikati ya Jiji, wakafanyie biashara zao katika maeneo mengine ikiwemo ya Buhongwa, Mkolani, Igoma na Nyegezi.

Jana polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya machinga katika eneo hilo ambapo machinga walikuwa wakilalamika kuondolewa katika eneo hilo bila kushirikishwa licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku machinga kubugudhiwa.
Machinga katika eneo hilo ambapo machinga walikuwa wakilalamika kuondolewa katika eneo hilo bila kushirikishwa licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku machinga kubugudhiwa.
Uchochoro wa Msikiti wa Temple Makoroboi Jijini Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.