LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YAANZA UTAFITI KUANGAZIA HALI YA UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME HUSUSANI MAENEO YA VIJIJINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Serikali kupitia wakala wa nishati Tanzania (REA) pamoja na ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) imeanza utafiti wa kuangalia hali
ya upatikanaji wa nishati nchini hususani katika maeneo ya vijijini katika mikoa 26 ya Tanzania bara kuanzia Oktoba 10 hadi Novemba 15 mwaka huu.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es salaam Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt.Ephraim Kwesigabo, na kwamba lengo la utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa Nishati umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya ili kujua matumizi ya umeme na nishati pamoja na faida zake kwa maendeleo.

Sambamba na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago alisema kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wana kaya zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo yao.

Aidha, alisema kuwa timu ya wadadisi wapatao 130 watahusika katika zoezi hilo la ukusanyaji taarifa ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja na wataalamu wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya takwimu makao makuu

Pia taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Mbali na hayo wananchi wameombwa kutochukua sheria mkononi kwa kuwadhuru watafiti wanapokuwa wakifanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kupata takwimu rasmi
zinazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya
maendeleo.

No comments:

Powered by Blogger.