LIVE STREAM ADS

Header Ads

BODABODA MWANZA WAANZA KUNYOOSHANA ILI KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umeanza mikakati ya kusaidia mapambano dhidi ya ajali za barabarani ambazo wakati mwingine husababishwa na uzembe wa baadhi ya waendesha bodaboda.

Akizungumza na Lake Fm, Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Seif Kagoma, amesema miongoni mwa mikakati iliyopo ni kuhakikisha bodaboda wote wenye sifa ikiwemo kuwa na leseni wanasajiliwa pamoja na kushirikiana na vyombo vya usalama kuwakamata bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.

Amesema vijana wengi wanaoingia kwenye uendeshaji wa bodaboda huwa hawana uelewa wa kutosha katika kuzingatia sheria za usalama barabarani na huwachukua muda mrefu hadi kuzingatia sheria hizo jambo ambalo limesababisha malalamiko yasiyoisha dhidi ya bodaboda.

Kagoma amewahimiza waendesha bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutotumia vileo wakati wa kazi pamoja na kujiepusha na mwendo kasi hatua ambayo itasaidia kupambana na ajali za barabarani.

No comments:

Powered by Blogger.