LIVE STREAM ADS

Header Ads

EBWANAEEEEE DAR ES SALAAM TIGO FIESTA 2016 LEO IMOOOOOO!

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kushoto), akisalimiana na msanii Snura Mushi alipokuwa amewasili jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Kampuni ya Simu ya Tigo kuzungumza na wanahabari wakati akijitambulisha kwao  Dar es Salaam kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika leo katika Viwanja vya Leaders Klabu Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kulia), akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii wa hapa nchini na kutoka Nigeria ambao watatoa burudani leo katika viwanja vya Leaders.
 Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kulia) , akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika leo viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii mwenzake, Tecnomile na katikati ni msanii Snura Mushi.
 Msanii Tecnomile (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Huduma wa Masoko wa Tigo, Olivier Prentout.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikipigwa na msanii Tecnomile.
***********************************
Na Dotto Mwaibale

WASANII Yemi Alade na Tecnomile kutoka Nigeria leo watapanda jukwaani na washindi 16 washindano la Tigo Fiesta 
Super Nyota katika fainali ya Tamasha la Fiesta 2016 lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika mkutano wa kujitambulisha kwa wanahabari msanii Tecnomile alisema Tanzania kwake ni kama nyumbani na Diamond na Vanesa  ni washikaji zake hivyo atatoa burudani kali ili washikaji wakumbuke ujio wake.



Kwa upande wake msanii Yemi ameshukuru mapokezi makubwa yaliyofanywa dhidi yao na kuwa anaipenda Tanzania na anajisikia 

yupo nyumbani na pia anakipenda Kiswahili.


Yemi alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hasa wapenzi wa muziki kufika kwa wingi katika viwanja hivyo kupata burudani la kukata na shoka.



Tamasha la Tigo Fiesta 2016  limekuwa  likiendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania 

huku Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.

No comments:

Powered by Blogger.