LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAZOEZI MUHIMU YA KUFANYA NYAKATI ZA ASUBUHI.

Nyoosha viungo
Hii itakusaidia kuweka viungo vizuri wakati ambapo umetoka kuamka kwa sababu sehemu kubwa ya viungo vya vitakuwa vimejiweka kwenye postion moja kwa muda mrefu hivyo ni vizuri kuvinyoosha ili viwe tayari kwa mkao wa mazoezi. nyoosha viungo kwa dakika 10 kisha anza mazoezi.


Viungo vya kunyoosha ni kama magoti, shingo kwa kuizungusha kulia na kushotp, mabega kwa kuzungusha mkono wako kulia na kushoto, enka na kiuno.

Ruka ruka
Hii husaidia kuweka mzunguko wa damu vizuri pia husaidia kufanya moyo uweze kusambaza damu sehemu mbalimbali kwa kasi pia husaidia mfumo wa kutia taka mwili kama figo na ngozi kutoa taka mwili vizuri. Hupunguza mzigo wa figo kuchuja damu kwa kufanya mwili kutoka jasho kwa wingi hivyo taka mwili kama chumvi chumvi kutoka.

Ruka kichura
Hii husaidia kukaza misuli ya miguuni na kufanya misuli hiyo iwe na nguvu  kisha kimbia kwa mwendo wa kawaida kwa muda wa dakika 20 ili kuweza kufanya mapafu yako yawe imara pia viongo vyote vya mwili hushiriki katika zoezi hili la kukimbia.

Kaza misuli ya tumbo
Hii hufanyika kwa kulala chini kwa mgongo kisha kunja miguu yako na nyanyua kiwiliwili kisha gusisha kiwiliwili na magoti fanya hivyo 10 au 15 kisha pumzika hii husaidia kukata tumbo na kuweka misuli yako ya tumbo katika hali ya uimara.

Mwisho
Kwa kufanya hivyo utakuwa umeweza kufanya mwilli wako kuwa pouwaa kwa kuhakikisha kwamba kila kiungo cha mwili kimefanyiwa zoezi mwisho kabisa nyoosha viungo  tena kisha ingia bafuni oga na endelea na shughuli zako. Usizidishe lisaa limoja katika mazoezi yako.

BMG/Mtandaoni

No comments:

Powered by Blogger.