LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA MALI IKO SHAMBANI

"Niko katika shamba langu la mahindi lililopo Kenyamanyori, Tarime mkoani Mara. Mbali na kazi za kuipasha jamii habari, mimi napenda sana shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Ni kazi ambayo hata mzee wangu (apumzike kwa amani), ilimjengea heshima kubwa. Nilijifunza kilimo kutoka kwake.

Kazi ya kilimo inalipa ukiifanya kwa moyo wa dhati licha ya changamoto za pembejeo zilizopo nchini.

Serikali na wadau mbalimbali wa kilimo, wasaidie kutatua changamoto za kilimo ili kitoe changamoto ya ajira kwa vijana." George Binagi, Mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na Mwanablogu wa BMG.

No comments:

Powered by Blogger.