LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA AFYA KUWA MGENI RASMI KWENYE KONGAMANO KITAIFA LA AFYA JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161111_093640.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la kitaifa la afya litakalofanyika Novemba 14 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Jana Rais wa Kamati ya maandalizi  ya mkutano huo, Dkt. Omary Chillo alisema lengo lake ni kujadili maendeleo ya sekta afya nchini.

Aidha Dkt. Chillo alisema kuwa  kongamano hilo litajadili jitihada ilizofikia Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimkakati ya maisha yenye afya njema (SDG-3) yaliyokusudiwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya wachapakazi.

Dkt. Chillo aliongeza kuwa kongamano hilo pia linatarajia kujadili mikakati ya kuboresha sheria ya usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi nchini kwa  ajili ya maendeleo ya wafanyakazi na usalama wao.

Kwa mujibu wa Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo pia linatarajiwa kufanyika kuwakutanisha wataalam wa sekta ya afya 700 na kuratibiwa na taasisi tano zikiwemo MoHCDGEC, TMHS,APHFTA,CSSC na BAKWATA.

Mkutano  huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya, zinatarajia pia  kushiriki katika maonesho  ya bidhaa zinafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.

No comments:

Powered by Blogger.