AGIZO LA JPM KUHUSU MACHINGA MWANZA LIWE FUNZO KWA VIONGO.

Anaandika: Edwin Soko
0754551306
Maamuzi ya Rais kutengua maamuzi ya kufukuzwa kwa Wamachinga
Wengi tumesikia kauli ya Mh. Rais juu ya kurudishwa kwa Wamachinga kwenye mitaa na vitongoji vya Jiji la Mwanza.
Ni wazi kuwa kauli hiyo umehamsha furaha kwa Wamachinga wengi na kuleta maumivu wa watendaji ya Serikali, kama mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya, na Wakurugenzi wa halmashauri za Nyamagana na Ilemela.
Niliandika kwenye makala yangu ya mtandaoni niliyoipost siku tatu zilizopita kuwa, suluhu ya wamachinga na viongozi wa Jiji la Mwanza ni maridhiano(Reconciliation) na nilifanya nukuu ya mzee wetu Mandela.
Katika hoja zangu nilisimamia uwepo wa nia njema ya Viongozi wa Mwanza kwenye kuliweka Jiji safi, lakini nilitoa angalizo kuwa, zana mpya ya utawala (New management mode) inajikita kwenye kuyabadilisha mazingira kulingana na hali iliyopo na sio hali iliyopo itufanye kuyakimbia mazingira.
Hapo nilipendekeza kuona nia ya kuyaboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuyarasimisha kuwa kwenye mfumo rasmi ili wachangie kodi. Nilidokeza umuhimu wa kuiga yale yanayofanywa na Nchi nyingine kama kufunga barabara kwa muda fulani ili wamachinga wafanye biashara na kuchangia uchumi wa Nchi.
Kutoepukika kwa kauli ya Mhe. Rais
Kauli ya Mh. Rais isingeepukika kwani, anasoma historia yake ya kuingia madarakani kulivyochangiwa na wananchi wa kawaida wenye maisha ya chini kabisa, kwani walimchagua ili awe mtetezi wa wanyonge, hivyo kutotekeleza hilo kungesababisha kupoteza imani kwa wapiga kura wake, wakati yeye mlengo wake ni kuwa sauti ya wanyonge.Maamuzi yake yatasaidia kwa kiasi fulani kuokoa jahazi la CCM kwenye uchaguzi ujao 2020.
Kauli ya Rais yathibitisha kufa kwa mfumo wa utawala Serikalini (Institutional framework vacuum)
Kwa mujibu wa madaraka ya kikatiba ibara ya 33 Rais ni mtu mwenye maamuzi makubwa analindwa kisheria hivyo anaweza kutoa maamuzi yoyote yale yenye maslahi ya Taifa, lakini maamuzi ya leo yameleta picha tofauti sana.
Hivi inawezekana vipi kuwa, na serikali moja ya chama kimoja lakini ikawa na mkizano wa maamuzi, yaani wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wakasema kauli nyingine na Rais akaja na kauli nyingine?
Hii haina tija sana kichama, na inaweza kutumiwa kama moja ya madhaifu makubwa kwa serikali ya inayoongozwa na CCM, kwa ushauri wangu Serikali ijifunze kwa hili lililotokea, kwani matokeo yake ni mabaya sana ni wazi sasa watendaji wa chini wanaomsaidia Rais hawataheshimika na badala yake watu wataheshimu utawala wa juu na sio wa chini.(Up - down management)
Rai yangu:
Watendaji wa chini wasijisikie vibaya kwa hatua hiyo, huenda Mh. Rais ameliona kwa mapana zaidi pia kwa kuwa wao ni wateule basi waone nia njema ya Mh. Rais na chama chake kuwa huenda wamesoma alama za nyakati.
No comments: