LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YAFURAHISHWA NA MCHANGO WA BLOGGERS NCHINI, SASA KUANDALIWA TUZO MAALUMU.

#BMGHABARI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema serikali inatambua mchango wa waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini (Bloggers) hivyo itaendelea kushirikiana nao.

Waziri Nnauye ametoa kauli hiyo mchana wa leo Jijini Dar es salaam, wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Chama cha Waendesha Mitandao ya Kijamii nchini, (Tanzania Bloggers Network TBN) ulioanza jana kwa kutambuliwa na semina juu ya uendeshaji sahihi wa mitandao hiyo.

Amesema waendeshaji wa mitandao ya kijamii wanayo nafasi kubwa katika kuupasha umma habari hivyo serikali itaendelea kushirikiana nao ili kufanikisha adhma hiyo huku akiwakanya maafisa habari wa Serikali hususani mikoani kuacha tabia ya kutotoa ushirikiano dhidi ya bloggers pindi wawapo kazini.

Aidha amedokeza kwamba Serikali iko tayari kutunga kanuni za kuwatambua bloggers nchini katika sheria ya habari 2016 ili kufanikisha bloggers hao kupata vitambulisho vya wanahabari  "Press Cards".

Hata hivyo amedokeza kwamba mchango wa bloggers nchini ni mkubwa hivyo kupitia wadau wengine, hapo mwakani utaandaliwa utaratibu wa kutolewa tuzo kwa bloggers ili kutambua mchango wao.

Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, ametoa rai kwa waendesha mitandao ya kijamii nchini (bloggers) kujiunga na umoja huo ili kutambulika zaidi katika utendaji kazi wao.

Mkutano huo ulidhaminiwa na Benji ya NMB na wadau wengine wakiwemo PSPF, NHIF, Kampuni ya Bia Serengeti, Cocacola, ambapo kauli mbiu yake ni Mitandao ya Kijamii ni ajira, itumike kwa manufaa

No comments:

Powered by Blogger.