LIVE STREAM ADS

Header Ads

DHAMANA YA MKURUGENZI WA JAMII FORUMS.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

#lakefmhabari
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imemuachia kwa dhamana Mkurugenzi na mmiliki wa mtandao maarufu wa Jamii Forum, Maxence Melo, anayekabiliwa na kesi tatu.

Melo amepewa dhamana hiyo baada ya kukidhi masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili.

Ijumaa iliyopita alipelekwa rumande baada ya upande wa Jamhuri kuondoka mahakamani wakati akisubiri mdhamini mmoja ili kukamilisha taratibu za dhamana.

Melo anakabiliwa na kesi hizo tatu ambapo katika kesi ya kwanza anadaiwa kuzuia na kuharibu data ambazo jeshi la polisi wamekuwa wakizihitaji kwa ajili ya uchunguzi.

Katika kesi ya pili Melo anadaiwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kuharibu uchunguzi huku kosa la tatu likiwa ni kumiliki tovuti ambayo haina miliki ya tanzania.
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo desemba 29 mwaka huu.

No comments:

Powered by Blogger.