LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AZINDUA MAZOEZI YA KITAIFA KWA VIJANA MKOANI KAGERA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  wa tatu kulia akiongoza zoezi la jogging wilaya karagwe pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (katikati) akiendeleza zoezi la jogging pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Kagera Yahaya Kateme (kusho) pamoja na viongozi na wanachama wengine.
Na Fahadin Siraji
Kaimu katibu mkuu Uvccm Taifa, Shaka Hamdu Shaka leo amezindua rasmi kampeni ya mazoezi ya mwili(Jogging UVCCM) yenye kauli mbiu ya "MAZOEZI KWA AFYA" iliyozinduliwa kitaifa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Shaka ameongozana na Mwenyekiti  Uvccm mkoa wa Kagera, Yahya Kateme, Mkuu wa Wilaya Karagwe, Godfrey Ayub Mheluka pamoja na vijana na viongozi mbalimbali  Wa Chama na Serikali Wilayani humo.  

Akiongea baada ya mazoezi hayo, Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM ngazi za wilaya nchini kote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa tangu tarehe 24 mwezi Oktoba mwaka huu ya kuanzisha klabu za mazoezi (Jogging Club).

"Nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa mazoezi, sasa vijana lazima wawe wakakamavu na tayari muda wote hatuwezi kuwa na taifa la vijana goigoi wasio jiweza kama ambavyo  hata makamu wa rais alivyounga mkono katika swala hili la mazoezi". Alisema Shaka.

Amesema Jogging ni suala muhimu kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yao kuwa imara, huwafanya kuwa wamoja wenye ushirikiano wa kudumu hususani katika mambo mbalimbali ya kijamii'.

Shaka yuko katika ziara ya siku nane mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote nane za mkoa huo.

No comments:

Powered by Blogger.