MGOMBEA UBUNGE ACT WAZALENDO JIMBO LA MOROGORO AACHANA NA CHAMA HICHO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


#BMGHabari
Akiyekuwa mgombea bunge 2015 Jimbo la Morogoro kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Seleman Msindi (Afande Sele, kulia) leo ametangaza rasmi kujiondoa ndani ya chama hicho huku akishindwa kuainisha sababu za kufanya hivyo.
Maamuzi hayo yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka taarifa za za Afande Sele kuachana na chama chake ambapo habari hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo amebainisha kwamba kuanzia sasa siyo mfuasi wa chama chochote cha siasa.
"Naomba ieleweke kuwa uamuzi huu 'tarajiwa' sijauchukua kwa bahati mbaya hivyo naomba kila mmoja awe wa ndani au wa nje ya chama chetu aheshimu uamuzi wangu kama mimi ninavyoheshimu maamuzi ya watu wengine kwa mujibu wa katiba ya nchi inavyosema...Ahsanteni sana wadau tukutane maishani". Imeeleza sehemu ya taarifa ya Afande Sele ambaye pia ni mkongwe wa mziki wa Hip Hop nchini, kwenye ukurasa wake wa facebook.
No comments: