LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI NAPE NNAUYE AIPONGEZA TBN KWA UPASHAJI WA HABARI NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Dar es Salaam, WAZIRI wa habari na Uenezi, Nape Nauye, amesema siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingia madarakani ni mitandao ya kijamii.
Akifunga jana kongamano la mkutano mkuu wa Umoja wa Wanachama wa mitandao ya kijamii (blogeers), Nape alisema CCM imeingia madarakani baada ya kuandikwa kwa upana mkubwa katika mitandao ya kijamii.
Alisema mitandao ya kijamii iko na nafasi kubwa katika jamii ambapo asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia mitandao ya kijamii ambapo habari nyingi wakati wa kampeni walikuwa wakisoma katika mitandao hiyo.
“Leo nitoe siri kwenu kuwa CCM kuingia madarakani ni ninyi mabloggers, hivyo nawapongezeni na niko nanyi bega kwa bega” alisema Nauye
Aliitaka mitandao hiyo kufuata maadili ya upashaji habari na kuepuka upotoshaji jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa jamii hivyo kuwataka kuzingatia taaluma hiyo.
Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie na Waziri wa habari na Uenezi mara baada ya kufunga kongamano la mkutano mkuu wa mwaka wa Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam jana.

No comments:

Powered by Blogger.