MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu mkoa wa Dar es salaam, Paulo Makonda, jana amefanya ziara
kukagua ujenzi unaoendelea katika hospital ya mama na mtoto iliyopo eneo la Chanika na ambayo itawahudumia wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani waliokuwa
wakilazimaka kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali ya Amana na Muhimbili.
Akizungumza mara baada ya kukagua hospitali hiyo Makonda
alisema kuwa hospitali hiyo itakuwa na vitanda 160 na itakuwa inahudumia
wagojwa 1000 kwa siku, na vikiwa na vyumba viwili vya upasuaji vyenye
uwezo wa kuhudumia wagonjwa wagonjwa wanne kwa kila chumba huku
kukiwa na Watumishi zaidi ya 150 ambao watakuwa wakiishi hapo hapo
karibu na hospitali hiyo kwani ujenzi wa hospitali hiyo unaendana na
makazi wa wafanyakazi.
"Nimeshangaa na kufurahi Mara baada ya kukuta ujenzi ukiwa
umefikia sehemu nzuri maana nilikuja kuweka jiwe la msingi mwezi wa tatu
mwaka huu na kwa muda uliopita ni wazi kabisa kazi inafanyika kwa
ufasaha mkubwa," alisema Makonda.
Mradi huo ambao umefadhiriwa na shirika la maendeleo ya
Korea ya kusia (KOICA), ukiwa umegharimu billion nane na million mia nane
mpka kukamilika kwake na unategemewa kukamilika mwezi februari mwakani.
No comments: