LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biashara ya Ngono kwa Watoto Migodi ya Msalala Yawashtua Wanaharakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com

Mtemi wa Jeshi la Jadi Sungusungu kijiji cha Lunguya, Julius Kahenyela Manyama 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuanzia mwaka 2020 hadi 2022 kuhusu ukatili wa kijinsia ambapo miongoni mwa mijadala iliyotawala ni pamoja kuwepo kwa Biashara haramu ya Ngono maarufu ‘Mchemsho’ kwenye migodi ya Nyamishiga, Kalole na Nyangalata inayofanywa na watoto wadogo na watu wazima.


Mkutano huo umefanyika Jumatano Novemba 16,2022 na kukutanisha makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo watu maarufu, waganga wa jadi,Wakango, viongozi wa dini, mila, serikali, sungusungu, vijana, wanafunzi na kituo cha taarifa na maarifa Lunguya.

Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi amesema Lengo la Mkutano huo ni kujadili hali halisi ya ukatili wa kijinsia kabla na baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya mwaka 2020 na Namna kituo cha taarifa na maarifa kinavyoshirikiana na jamii na serikali katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia.

Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manuari amesema hali ya sasa tofauti ni kubwa sana ambapo masuala ya mimba za wanafunzi yamepungua, utoro umepungua na ukatili umepungua.


“Pamoja na uwepo wa migodi lakini vijana wetu wanajitambua wameshajua wafanye nini, tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wanajua ni kuolewa tu, hawakujua madhara ya mimba za utotoni kwa kweli mabadiliko ni makubwa, watoto wameshajitambua”,amesema Manuari.
Mmoja wa wanafunzi akizungumza kwenye mkutano

Wanafunzi walioshiriki mkutano huo wamesema awali walikuwa wanaachishwa shule, wanafunzi walikuwa wanatoka umbali mrefu kwenda shule, watoto wa kike hawakupewa nafasi ya kwenda shule na wengine walikuwa wanabakwa lakini sasa hali imebadilika mambo yanaenda vizuri.

Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza amesema tofauti na hapo awali hivi sasa Wanawake wanashiriki kwenye machimbo kama wanaume, wakango wamepunguza matusi na wanaendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.


Licha ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa ikiwemo kupungua kwa mimba na ndoa za utotoni, utoro shuleni, wanawake kunyanyaswa lakini suala la Biashara ya ngono kwenye maeneo ya migodi inayofanyika kati ya wasichana wadogo na wanaume watu wazima lakini pia akina mama watu wazima na wavulana wadogo kwa gharama ya shilingi 3,000/= imetajwa kuwa changamoto kubwa inayosababisha mmomonyoko wa maadili na kuchochea ukatili wa kijinsia.
Bi. Mariam Paul Kadushi 

Mmoja wa Washiriki wa mkutano huo Bi. Mariam Paul Kadushi ambaye ni mwanakituo cha Taarifa na maarifa Lunguya ameeleza kusikitishwa na biashara ya ngono inayoendelea kwenye migodi ya dhahabu iliyopo katika kata ya Lunguya ambapo mabinti wadogo wamekuwa wakiuza miili yao kwa wanaume wanaofanya kazi ya uchimbaji madini.

“Watoto wetu hawapo salama sasa kwenye migodi, mabinti wadogo wanafanya ngono na wababa watu wazima lakini pia vijana wetu wa kiume nao wanafanya ngono na akina mama watu wazima, haya mambo ya hovyo kabisa, naomba Jeshi la Jadi Sungusunguna serikali muingilie kati suala hili, akina baba wanachukua mali za familia na kwenda kuuza wapate pesa ya MCHEMSHO (kufanya ngono)”,amesema Bi. Mariam.

Naye Bi. Mgaile Bundala amewataka wazazi kusimama imara kwenye suala la malezi ya watoto huku akiwashauri akina mama waliokengeuka na kujihusisha na mapenzi na vijana wadogo kuachana na vitendo hivyo. 

“Mtoto anaenda kujipanga mchemsho atakulea kweli ukizeeka, siamini kama watoto watatutunza uzeeni. Zamani wakati wa nyuma tulikuwa na shikome, tulikuwa tunakaa na kujadili, tunawakanya, siku hizi jioni jioni watu wapo kwenye kahawa,wapo tu mtaani. Utandawazi umezidi mno. Wavulana wadogo wanachemsha na wamama wakubwa mgodini, mabinti wadogo nao wanachemsha na wababa watu wazima, huu ni mmomonyoko mkubwa wa maadili”,amesema Bi. Mgaile.
Mwana kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya Mlima Emmanuel.

Kwa upande wake Mwana kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya Mlima Emmanuel amesema amefuatilia biashara ya ngono maarufu “Kuchemsha/Mchemsho” na kubaini kuwa vijana wadogo wa kike wanajihusisha na biashara hiyo haramu kwa shilingi 3,000/=.

“Ni hatari sana, mabinti wadogo wanafanya ngono na akina baba wakubwa kabisa, akina mama watu wazima nao wanafanya ngono na vijana wadogo wa kiume, naomba serikali isaidie kukomesha jambo hili kwani ni chanzo cha ukatili wa kijinsia”,amesema Emmanuel.

“Wakati wa mavuno wanaume wanatumia mali za nyumbani kwenda kwenye Mchemsho. Vijana wanafanya mapenzi na watu wazima, watu wazima nao wanafanya ngono na watoto wadogo. Naomba tudhibiti janga hili la mchemsho, tuchukue hatua kwa sababu tunapoteza mali za familia kwani akina baba wanahujumu mali walizotafuta na wake zao nyumbani pia kuna magonjwa ya ngono”,ameongeza kijana Kishanda Lucas Matemela.


“Sisi wazazi tujitambue ili iwe rahisi kuwarekebisha watoto, pamoja na utandawazi uliopo lazima tubadilike, utandawazi umetukuta. Sisi hatujapitwa na wakati sisi tupo kwenye wakati, mambo yote yanayofanyika sasa hivi ni marudio, tukae na watoto wetu tuzungumze nao, tukisema hawatusikii kweli hawatatusikia kweli, hata haya ya Mchemsho yataisha. Usichoke kutoa ushauri, tukae na vijana tuwaambie, watatusikiliza”,amesema Mwalimu Moris Shayo.

Kwa upande Mtemi wa Jeshi la Jadi Sungusungu kijiji cha Lunguya, Julius Kahenyela Manyama amesema ni kweli amesikia kuhusu Mchemsho na changamoto inayotokea pindi wakitaka kushughulikia tatizo hilo wanaonekana kuingilia uhuru wa wachimbaji migodini.

“Mambo ya mchemsho yapo machimboni, watu wanatoka maeneo mbalimbali nchini kwenda kufanya biashara hiyo haramu, huku vijijini hiyo biashara haipo ni vyema viongozi wa maeneo husika wakalifanyia kazi jambo hilo. Hata hivyo Vijana wanasema sisi wazee tumepitwa na wakati, wakati sisi tumeona mambo mengi tu. Tukiwashughulikia wanasema sisi ni tatizo”,amesema Manyama.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu, Fredina Makeleja Said amewataka Wazazi wasiogope kuzungumza na watoto wao kwani watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili na hawasemi.

“Watoto wetu wafanyiwa ukatili na watu wa karibu, ndugu lakini kama huzungumzi na mtoto huwezi kujua mambo anayopitia mwanao, mfano kuna vitendo vya ulawiti watoto wanafanyiwa nyumbani, shuleni lakini huwezi jua kama huzungumzi na mtoto. Tunatakiwa tubadilike kwa sababu madhara yaliyopo kwa vijana ni makubwa, tusiposema tutaharibu jamii yetu”,amesema Fredina.

Kaimu Afisa Mtendaji kata ya Lunguya Peter Mgosi Madamanya amesema msingi wa malezi ya watoto unaanzia katika ngazi ya familia hivyo ni lazima kuwe na mkazo wa malezi kuanzia ngazi ya familia ili kulinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu, Fredina Makeleja Said akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya ya Kishapu, Fredina Makeleja Said akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya, Loyce Kabanza akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP) Aluwa Hamisi Mkilindi akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manuari akizungumza kwenye Mkutano wa Tathmini ya kazi zilizofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na wanajamii kuhusu ukatili wa kijinsia 
Wanajamiii wakiwa kwenye Mkutano
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Lunguya Meja Masalu akielezea kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mwalimu Moris Shayo akichangia hoja wakati wa mkutano huo
Mgaile Bundala akichangia hoja wakati wa mkutano huo
Afisa Mtendaji kijiji cha Madaho kata ya Lunguya, Oliver Kafumu akizungumza kwenye mkutano
Mwezeshaji kutoka TGNP Sylvia Sostenes akizungumza kwenye mkutano huo
Mwezeshaji kutoka TGNP Sylvia Sostenes akizungumza kwenye mkutano huo
Kaimu Afisa Mtendaji kata ya Lunguya Peter Mgosi Madamanya akizungumza kwenye mkutano
Kishanda Lucas Matemela akizungumza kwenye mkutano
Junior John akizungumza kwenye mkutano
Mdau akizungumza kwenye mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye Mkutano
Mdau akizungumza kwenye mkutano
Mdau akizungumza kwenye mkutano

Mdau akizungumza kwenye mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye Mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye Mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye Mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi
Wanajamiii wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi
Wanajamiii wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi
Wanafunzi wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi
Wanajamiii wakiwa kwenye majadiliano ya kikundi
Wanajamiii wakiwa kwenye mkutano
Viongozi na Wanajamiii wakiwa kwenye mkutano
Viongozi na Wanajamiii wakiwa kwenye mkutano
Wanajamiii wakiwa kwenye mkutano
Mdau akizungumza kwenye mkutano
Mdau akizungumza kwenye mkutano
Washiriki wakiwa kwenye mkutano

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments:

Powered by Blogger.