LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA "NI HEKIMA PEKEE" LA JIJINI MWANZA LAWAHIMIZA WANAOTOKA KAYA MASKINI KUFANYA KAZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand,Mwanza
Wakazi wanaotoka kaya maskini na wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ( VVU) Jijini Mwanza, wamehimizwa kujishughulisha kwa kufanya kazi kwa bidii, ili kujiinua kiuchumi na kuacha kutegemea misaada ya watu mbalimbali ikiwemo serikali.

Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali  la Ni Hekima Pekee, linalojishughulisha   kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na familia duni Onesmo Kajuna, wakati akitoa msaada wa Sh. 350,000 kwa kikundi cha Uvumilivu  kilichopo mtaa wa Kageye kata ya Lwanhima wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kajuna alisema lengo la kutoa fedha hizo kwenye kikundi hicho, ni kusaidia ili waweze kujikwamua kiuchumi katika familia zao  na kuepuka kuwa tegemezi.

“fedha hizi  zimetolewa  na Halmashauri ya jiji la Mwanza, kitengo cha Ukimwi ambazo ni ruzuku kwa mashirika binafsi yanayosaidia jamii , hivyo tunatambua zitawasaidia  kuongeza mitaji kwenye biashara zao na kujikwamua kiuchumi sambamba na kupeleka watoto wao shule, kununua lishe kwa ajili ya kuboresha afya zao,kwani asilimia 80  ya wanakikundi hiki  ni wajane," alisema Kajuna.

Pia aliwaomba wananchi  kuchangamkia  fursa zinazotolewa na mashirika mbalimbali ili kujiinua kiuchumi, sambamba na  kushirikiana nao katika  kuwajengea uwezo na kuwashauri  kwani  kupata maradhi siyo  mwisho wa maisha.

Naye Mwenyekiti wa  mtaa wa Kageye Tumaini Andrew alisema, atahakikisha anawahamasisha wanakukindi hao, kuzalisha fedha hizo na kurejesha  mkopo na riba kwa wakati,na faida itakayopatina itatumika kununulia mahitaji yao ikiwemo lishe.

“Naamini fedha hizo,  watazitumia vizuri, kwani kila  baada ya miezi sita tutakuwa tukiangalia  faida iliyopatikana,itakayo tumika kununulia lishe kwa ajili ya kuboresha afya zao na nyingine   zitawasaidia  kuwapeleka watoto shule,”alisema Andrew

Kwa upande wa  Katibu wa kukindi hicho Monica Philipo, aliishukuru shirika hilo kwa kuwapa msaada huo, na kuahidi kuzitumia vizuri  kwa kufanya biashara  ambazo zitawaongezea   mtaji.

“Kila wanakikundi atafanya biashara zake ikiwa na lengo la  kuhamasisha katika kujishughulisha na kuepuka kuwa tegemezi kufanya hivyo kutapunguza  wakina mama  kukaa bila kazi,”alisema Philipo.

Naye Ofisa  Mtendaji wa Kata Lwanhima, Navatus Kayingiriza alisema watu wakijishughulisha kwa kufanya kazi  kutapunguza ongezeko la maambukizi ya  VVU, kwani  kujituma kwa bidii  kutasaidia kukuza uchimi katika familia zao.

No comments:

Powered by Blogger.