LIVE STREAM ADS

Header Ads

DAWA ZA KULEVYA ZAMCHACHAFYA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, Dar
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataja watuhumiwa wa kuuza dawa za kulevya na watumiaji wakiwemo maofisa tisa wa jeshi la polisi mkoani humo.

Miongoni mwa wakuu waliotajwa ni pamoja na Christopher Fuime ambaye alikuwa mkuu wa polisi wilaya ya Kinondoni pamoja na watu maarufu nchini ambao pamoja na aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu.

Akizungumza leo na wandishi wa habari ofisini kwake, Makonda alisema amefanya opareshenu usiku kucha na kubaini sehemu ambazo zinahusika na uuzaji wa dawa hizo na kuwataja majina kama Bakari Mohamedi Nassor, Nasor Mohamed Nasor, Said Masudi alimaarufu kama Alteza.

Aidha Makonda alimuonya Kamanda Simon Sirro akisema kama jeshi la polisi limeshindwa kufanya kazi litakuwa limepoteza sifa yake na kwamba yuko tayari kupoteza maisha na nafasi yake ya ukuu wa mkoa kwa kuongea ukweli.

Kama hiyo haitoshi, Makonda alitoa siku saba kwa vijiwe vyote na maeneo yote yanayouza dawa za kulevya kuachana na biashara hiyo mara moja.

No comments:

Powered by Blogger.