LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONGAMANO LA KUPINGA BIASHARA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KUFANYIKA LEO JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Tushauriane kupitia 0756 3915 06. Mabadiliko ni Sasa, Piga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya.
#LakeFmHabari
Vijana Wazalendo mkoani Mwanza kupitia taasisi ya Chinga Respect Complex, wameandaa kongamano la kujadili namna ya kupambana na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Kongamano hilo linafanyika hii leo kuanzia majira ya saa tano kamili asubuhi katika Ukumbi wa Kipepeo uliopo New Mwanza Hotel Jijini Mwanza na limelenga kuibua mawazo chanya kutoka kwa vijana ambao ni wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa hizo.

Mratibu wa kongamano hilo, Denis Kankono, amebainisha kwamba lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais John Magufuli pamoja na wateule wake akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, katika kuhakikisha matumizi na biashara ya dawa za kulevya vinatokomezwa nchini.

Vijana na viongozi kutoka taasisi mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo za elimu, dini, serikali, machinga, madereva wa daladala pamoja na bodaboda wanatarajiwa kutoa mawazo yao katika kongamano hilo.

No comments:

Powered by Blogger.