LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUTANO MKUBWA WA INJILI KATIKA VIWANJA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia), akimkaribisha Mchungaji Fred Mitchell (kushoto) kutoka Canada ili kuhudumu kwenye mkutano huo. Katikati ni mkarimani kutoka EAGT Lumala Mpya.
#BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili kwenye viwanja vya kanisa hilo.

Ni mkutano uliojaaa Neema na miujinga ya roho mtakatifu ambapo watumishi wa Mungu kutoka Canada wakiongozwa na Mchungaji Fredy Mitchell wapo kwa ajili ya kutoa mafundisho ya neno la Mungu na kuwaombea watu wote.

Kwa jina la Yesu, wenye magonjwa watapona, pepo watateketezwa na wenye mikosi maishani itang’olewa. Njoo ushuhudie kwaya mbalimbali ikiwemo Havilah Gospel Singers pamoja na waimbaji kama Martha Baraka wanavyoutetemesha mkutano huo.

Mkutano ulianza jumatano tarehe 22 na utahitimishwa jumapili hii tarehe 26, 2017 hivyo hakikisha haukosi. Kumbuka muda ni kuanzia saa tisa kamili mchana.

Ili kufika kanisa la EAGT Lumala Mpya, panda magari ya Ilemela ama Airport kisha shuka kituo cha Sabasaba, tembea hatua chache hadi Soko Kuu la Sabasaba, uliza kwa Mchungaji Daniel Moses Kulola. Nyote mnakaribishwa. Picha za mkutano bonyeza hapa

No comments:

Powered by Blogger.