SHIRIKA LA EFG LABAINI MAPUNGUFU YA KIUSAWA KATIKA MASOKO YA JIJINI MWANZA.
Msaidizi wa kisheria wa shirika la EfG Jijini Mwanza, Ikupa Mwakisu, akifafanua kuhusu mradi wa kuongeza usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake katika masoko kwenye warsha kwa wanahabari inayofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili.
Jimmy Luhende kutoka Taasisi ya Utawala bora na Demokrasia nchini, ADLG ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo
Wanahabari wakiwa kwenye warsha hiyo
Warsha ikiendelea
#LakeFmHabarUtafiti uliofanywa na shirika la Equality for Growth EfG katika Masoko mbalimbali Jijini Mwanza umebaini kwamba hakuna usawa wa kijinsia kwenye maamuzi baina ya wanaume na wanawake kwenye Masoko hayo.
Hatua
hiyo inaelezwa kuchochea suala la ukatili wa kijinsia ikiwemo wanawake
kunyanyaswa kwenye masuala ya ulipaji ushuru pamoja na kufanyiwa maamuzi
katika shughuli zao za kibiashara.
Msaidizi wa
kisheria wa shirika la EfG Jijini Mwanza, Ikupa Mwakisu, ameyasema hayo
kwenye warsha kwa wanahabari juu ya haki za wafanyabiashara masokoni na
utoaji wa taarifa.
Amesema zaidi ya asilimia 90
ya wanawake katika Masoko ya Jiji la Mwanza ikiwemo Soko Kuu na Mwaloni
si viongozi katika Masoko hayo na hufanyiwa maamuzi na wanaume.
Warsha
hiyo imelenga kuwajengea uwezo wanahabari ili kutambua mbinu mbalimbali
za utoaji wa taarifa za matukio ya uvunjwaji wa haki za wafanyabiashara
katika masoko na kuongeza uelewa katika jamii juu ya haki za msingi za
wafanyabiashara hao hususani wanawake.
No comments: