LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA OJADACT YAUNGANA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT), kimeunga mkono hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kutaja baadhi ya majina ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Jana akizungumza na wanahabari, Makonda alitaja majina ya wasanii wakubwa wanaodaiwa kutumia dawa hizo pamoja na kuagiza kukamatwa kwa polisi tisa walioko kwenye mtandao wa usambazaji wa dawa za kulevya jijini humo.

Mwenyekiti wa OJADACT  Edwin Soko,  ametoa msimamo huo leo mkoani  Mwanza wakati akizungumza na wanahabari ambapo alisema hatua hiyo ni muhimu katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwani Jiji hilo  ambalo limekuwa kitovu cha uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo.

“Biashara ya dawa za kulevya hazistaili kufumbiwa macho  kwa sababu zina athari kubwa kwa jamii ikiwemo   kuathiri mwili  kiroho na kiakili  ambapo madhara hayo hutokana na utumia aji wa dawa hizo na endapo yakiachwa  yaendelee yanaweza kukwamisha ustawi wa taifa kuekea kwenye uchumi wa viwanda. 

“Tunapongeza kitendo hicho cha viongozi wetu kufikia hatua ya kuyataja hadharani majina ya wauzaji wa dawa za kulevya, kwasababu jambo hili siyo rahisi na haikuwezekana huko nyuma, kutokana na hili ni vyema Wakuu wa Mikoa mingine waanze kuchukua tahadhari ya kupambana na watu watakaohamia mikoani baada ya kutangaziwa vita jijini Dar es Salaam, kwahiyo Mwanza, Tanga, Arusha nao wajipange kupambana na wafanyabiashara hawa,” alisema Soko.

Akizungumzia kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini alisema,  siyo nzuri kwani kuna ongezeko kubwa la matumizi ya dawa za hizo, hivyo kuitaka jamii kushiriki kwa kuwaumbua wauzaji na wasambazaji kwasababu wanaishi katika maeneo yao  na siyo kuiachia serikali pekee.

“Matumizi ya bangi yameongezeka kwa asilimia 6.5  kwa mwaka 2015/16, ambapo watumiaji 247 walishikiliwa kwa tuhuma hizo na matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine na Cocaine nayo yameongezeka,” alisema Soko.

 OJADACT inasisitiza  haki itendeke katika kuwashughulikia,wale  watakaopatikana na hatia katika sakata hilo, la  biashara ya dawa za kulevya kiujumla kadri  sheria  ya kuthibiti  dawa za kulevya  ya mwaka 2015 inavyosema. 

No comments:

Powered by Blogger.