LIVE STREAM ADS

Header Ads

VYOMBO VYA HABARI NCHINI HAVISAIDII KUTOKOMEZA UMASKINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory
Imeelezwa kuwa habari zinazotangazwa na vyombo vya habari hapa nchini hazichangii ipasavyo juhudi za taifa katika kutokomeza umasikini miongoni mwa wananchi walio  wengi wanaoishi vijijini.

Akizungumza na wandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam, mwanachama wa kituo cha sheria na Haki za binadamu (LHRC), Ananilea NKya  alisema utafiti umehusisha habari za 10,371 zilizotangazwa katika vyombo vya habari 15 katika muda wa mwezi mzima wa febuari  2014 ambapo utafiti umeonesha kuwa kati ya habari 10,371 zilizochapishwa  4,750 sawa na 45.8% zilitokea Dar es salaam na 5,621 sawa 54.2%  zilitokea mikoani na Zanzibar.

Aidha alisema kuwa utafiti huo unaonyesha kuwa habari zinazotangazwa na vyombo  vya hanabari vya kitaifa zinajihusisha na zaidi na maendeleo ya wanasiasa kwa sababu habari zinanukuu wanasiasa  ndizo zinapewa umuhimu mkubwa zaidi katika vyombo vya habari huku utafiti ukionyesha habari zilitawaliwa na mfumo dume  ambapo kati ya watu 14,655 walionukuliwa katika taarifa  10,371 wanawake  walikuwa  2,646 sawa na 18%/  huku wanaume  wakiwa 12,009 sawa na 82% .

Aliongeza kuwa Kati ya habari 411 zilizotangazwa kama habari kuu  katika vyombo hivyo 15 habari 234 nilikuwa za kisiasa ,121 zilijadili masuala ya kijamii na 56 uchumi  hii ikiwa na maana kwamba vyombo vya habari haviyapi umuhimu masuala ya kiuchumi ambayo ndiyo yanawafanya wananchi wengi kuwa masikini.

No comments:

Powered by Blogger.