LIVE STREAM ADS

Header Ads

BARAZA KUU CUF LAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limekutana Jijini Dar es salaam kwa ajiri  ya kujadili na kufanya uteuzi wa majina ya wagombea wa bunge la AfriKa Mashariki yatakaopelekwa kwa Katibu wa  bunge ili kupigiwa kura na bunge la Muungano wa Tanzania

Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba, jana alisema baraza litafuata taratibu zilizotolewa na Katibu wa bunge ambazo zinakitaka chama kuwa wazi ikiwa ni pamoja na kupeleka maombi ofisini au kwa barua pepe.

Mbali na kuteua wagombea wa Afrika Mashariki, baraza litajadili hali ya kisiasa Tanzania bara na Tanzania Zanzibar ili kubaini dira ya chama hicho kwa wakati huu, huku likipitisha wakurugenzi wa chama hicho na kuteua  bodi mpya ya wadhamini ya chama hicho kwani iliyopo imemaliza muda wake.
Imeandaliwa na James Salvatory, BMG Dar

No comments:

Powered by Blogger.