LIVE STREAM ADS

Header Ads

DDA FOUNDATION YA JIJINI MWANZA YATEMBELEWA NA MARAFIKI KUTOKA CANADA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya kulea watoto wenye uhitaji ikiwemo wa kielimu ya "Development Dreams Attainment Foundation-DDA Foundation", akizungumza juzi jumatatu baada ya wageni kutoka Canada ambao ni watumishi wa Mungu kuitembelea taasisi hiyo.

Waliokaa kushoto ni baadhi ya wazazi/ walezi wa watoto wanaolelewa kielimu na kiroho katika taasisi hiyo ya DDA Foundation iliyopo Kiseke A Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Wageni kutoka Canada ambao pia ni watumishi wa Mungu waliokuwa wakihudumu katika kanisa la EAGT Lumala Mpya kuanzia Februari 16 hadi Februari 26 mwaka huu ni Mchungaji Fred Mitchell, Karlin Mitchell, Joyce Dickson, Shirleen Weeks, Fredrica Walters na Barry Walters ambapo katika ugeni huo waliwasaidia watoto mahitaji mbalimbali ikiwemo mavazi na mahitaji ya shule.

Kila mmoja alifurahishwa na maono ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo na kuahidi ushirikiano wake katika kuhakikisha malengo na matarajio ikiwemo kuwasaidia watoto wanaolelewa na DDA Foundation ikiwemo kupata elimu yanafikiwa.
#BMGHabari
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akizungumza kwenye halfa hiyo
Kulia ni Mama Mchungaji, Mercy Kulola, akizungumza kwenye halfa hiyo. Kushoto ni Meneja wa taasisi hiyo ya DDA Foundation, Moses Daniel.
Baadhi ya viongozi wa DDA Foundation
Kushoto ni Mchungaji Fred Mitchell kutoka Canada, akizungumza kwenye halfa hiyo. Katikati ni Mchungaji Daniel Kulola na kulia ni Mama Mchungaji Mercy Kulola.
Waliokaa ni wageni kutoka Canada ambapo kutoka kulia ni Mchungaji Barry Walters na mkewe Fredrica Walters, wanaofuata ni Missionary Sherlin Weeks na Joyce Dickson
Baadhi ya watoto wanaolelewa na taasisi ya DDA Foundation iliyopo Ilemela Jijini Mwanza
Baadhi ya wazazi/walezi wa watoto wanaolelewa na taasisi hiyo ya DDA Foundation.
Watoto wakikabidhiwa zawadi zao na wageni kutoka Canada
Watoto wakiendelea kupokea zawadi
Picha ya pamoja baina ya wageni, viongozi wa DDA Foundation, watoto pamoja na wazazi/ walezi wao
Picha ya pamoja baina ya wageni, viongozi wa DDA Foundation pamoja na watoto
Marafiki mbalimbali wanakaribishwa DDA Foundation iliyopo Kiseke A Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza ili kushirikiana katika kuhakikisha ndoto za watoto wenye uhitaji ikiwemo wa kielimu zinatimia maishani mwao.

No comments:

Powered by Blogger.