LIVE STREAM ADS

Header Ads

GARI LA SERIKALI LANASWA KWA TUHUMA ZA KUVUNJA SHERIA ZA USALAMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Askari wa usalama barabarani Jijini Dar es salaam, akimsimamisha dereva wa gari la serikali lenye nambari za usajili STL.2415 aliyelazimisha kupita eneo la mataa ya Kariakoo, Mtaa wa Congo wakati mataa katika eneo hilo yakionesha rangi nyekundu (vyombo vya moto vinapaswa kusimama).

"Hata kama ni gari la serikali lazima lifuate sheria za usalama barabani kama magari mengi, tena siku hizi traffic hawababaishwi kama zamani hata uwe nani wanakukamata tu ukivunja sheria". Mmoja wa watembea kwa miguu alisikika akimweleza mwenzao katika eneo hilo.
Askari huyo alitoa maelekezo yaliyoashiria kumshinikiza dereva huyo kuzingatia sheria za usalama barabarani na baadaye kumruhusu kuendelea na safari baada ya mataa kuwaka rangi ya kijana inayoruhusu vyombo vya moto kupita.

BMG inahimiza sheria za usalama barabarani kuzingatiwa na watumiaji wote wa barabara bila kujali nyadhfa zao huku pia maaskari wa usalama barabarani wakipaswa kutimiza majukumu yao bila hofu wala kumuonea mtu. 

Vinginevyo labda kama chombo cha moto ni cha dharua kama vile ambullance amba kwenye msafara ambayo hayo taratibu zake zajulikana wazi.

No comments:

Powered by Blogger.