LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA MABATI YA ALAF YA JIJINI MWANZA YANUFAIKA NA MAFUNZO KUJIIMARISHA ZAIDI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi na Mshauri wa vifaa vya kuezekea  wa kampuni ya Alaf Shailesh Tripathi, akiwasilisha mada katika mafunzo Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi yaliyofanyika Rock City Mall Jijini Mwanza.
Judith Ferdinand, BMG
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo

Kampuni  ya  Alaf inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya kuezekea, ni miongoni mwa wadau  wa ujenzi, walionufaika na mafunzo endelevu ya 27 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi.

Mafunzo hayo yamefanyika wiki hii katika ukumbi wa Rocky City Mall jijini Mwanza, na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo Alaf.

Wakati akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Mkurugenzi na Mshauri wa vifaa vya kuezekea wa Alaf, Shailesh Tripathi amesema, wamepata fursa ya kuwaelekeza Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi bidhaa zilizopo na zinazozalishwa na makampuni mbalimbali likiwemo la kwao.

Tripathi amesema, pia wamepata kuelimishwa juu ya  sheria  namba 4 ya mwaka 2010 inayohusu sekta ya ujenzi na kutambua mambo yanayotakiwa kufuatwa.

Pia amesema, kampuni hiyo, itakua na kikao na  wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi, kwa ajili ya  kujadiliana kuhusu changamoto wanazozipata katika sekta ya ujenzi hasa katika suala la vifaa,ili wao kama kiwanda waweze kuzifanyia kazi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuendana na sayansi na teknolojia sambamba na soko la ushindani.

Naye  Mhandisi wa kampuni ya Alaf, Daudi Kidyamali, amesema, semina imewakutanisha na wadau mbalimbali  wa sekta ya ujenzi na kuweza kubadilishana uzoefu,kuelimisha jambo litakalosaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji bidhaa na kuwashauri wateja wao.

Aidha amewaomba, wataalamu hao kutumia na kuwashauri wateja wao kuchagua bidhaa bora katika shughuli za ujenzi, ili kupunguza gharama.

" Ujenzi ni gharama na siyo wa siku moja,hivyo nawaomba wadau wote wa ujenzi kutumia bidhaa bora,kwani sasa ni soko huria na bidhaa zipo nyingi, ili kuboresha kazi zao," amesema Kidyamali.

No comments:

Powered by Blogger.