LIVE STREAM ADS

Header Ads

MALENGO YA RAIS MSTAAFU, JAKAYA KIKWETE, KUPITIA TAASISI ALIYOIZINDUA LEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
James Salvatory, Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete leo amezindua rasmi taasisi  yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), yenye malengo ya kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne, ikiwemo afya, elimu, utawala bora na maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua taasisi hiyo, Dkt.Kikwete amesema kuwa bado anapenda kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo katika jamii na muda mrefu amekua akipenda kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu, hivyo taasisi hiyo itamsaidia katika kufikia malengo yake.

Pia amesema taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika kuondoa umaskini, mabadiliko ya hali ya nchi na kilimo kwa wakulima wadogo, huduma za afya, kutokomeza malaria na afya ya mama na mtoto.

Maeneo mengine ambayo taasisi hiyo inajihusisha nayo ni elimu kwa vijana ili kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo serikali inatoa huduma kwa wananchi.

Taasisi hiyo ina wajumbe tisa kutoka sehemu mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa akiwemo balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza Mukandala ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Profesa Willium Mahalu ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Utabibu Bugando.

No comments:

Powered by Blogger.