LIVE STREAM ADS

Header Ads

ALIYOYASEMA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM HII LEO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Halmashauri za mkoa wa Dar es salaam zimetakiwa kuangalia aina ya wakandarasi wanaoingia mikataba katika ujenzi wa miundombinu hasa barabara mkoani humo ili kuwezesha ujenzi na ukarabati wa barabara zenye viwango bora.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa mkoa huo. Paul Makonda, alipokuwa akizindua barabara ya Shimo la Udongo iliyopo Kurasini iliyokarabatiwa bure na kampuni ya Grand Tech Tanzania Limited kwa kiwango cha zege.

Aidha Makonda ameipongeza kampuni hiyo na kuishukuru kwa kuisaidia serikali katika juhudi za kuboresha mazingira ya mkoa wa Dar es salaam kwa kutengeneza miundombinu ya barabara ambayo itawaunganisha wakazi wa Kurasini na maeneo jirani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Liyaniva, ameishukuru kampuni iliyokarabati barabara hiyo na kuongeza kwamba hatua hiyo inasaidia utatuzi wa adha ya muda mrefu waliokuwa watumiaji wake.

No comments:

Powered by Blogger.