LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFADHILI KUTOKA NORWAY WAENDELEA KUKUTANA NA WADAU WANAOFANYA KAZI NA KIVULINI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Wafadhili kutoka nchini Norway wanaofadhili miradi ya kutokomeza ukatili wa kijinsia inaotekelezwa na Shirika la KIVULINI la jijini Mwanza, wameendelea kukutana na wadau mbalimbali wanaofanya kazi na shirika hilo ili kujifunza zaidi mbinu zinazotumika kuelimisha jamii.

Wafadhili hao kutoka shirika la FO, FOKUS na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania siku ya Jumanne Februari 10, 2026 walikutana na jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia la wanawake na watoto pamoja na maafisa ustawi na maendeleo ya jamii mkoani Mwanza.

Baada ya majadiliano ya pamoja, Mjumbe kutoka Kamati Tendaji ya Shirika la FO la nchini Norway, Ole Henrik Krakenes alieleza kuvutiwa na muundo wa dawati la polisi la jinsia na watoto Nyamagana hasa chumba maalumu cha usiri kwa ajili ya kushughulikia mashauri ya ukatili wa kijinsia. 

Pia Krakenes alisema wamejifunza jinsi maafisa ustawi na maendeleo ya jamii baada ya kujengewa uwezo na shirika la KIVULINI, wanavyosaidia kutoa elimu kwa jamii na kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi za chini kabisa kwenye jamii.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Janeth Shishila alisema mchango wa wadau wa maendeleo ikiwemo shirika la KIVULINI na wafadhili wao, umesaidia elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kufika katika makundi mbalimbali na kuboresha kamati za MTAKUWWA na hivyo kuleta matumaini ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.
Tazma Video hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.