LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANABINAGI WALIOZALIWA TAREHE TOFAUTI WAFANYA HAFLA YA PAMOJA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Pichani ni Kenny Zakaria Binagi (kushoto) pamoja na Elly Zakaria Binagi (kulia), wote wakazi wa Jijini Dar es salaam wakilishana keki hii leo jumapili March 19,2017 kwenye hafla ya kusherehekea kuzaliwa kwao iliyofanyika nyumbani kwao.

Elly alizaliwa March 18 na Kenny ni March 15 wote miaka tofauti iliyopita hivyo mwaka huu wakaona ni vyema wakasherehekea pamoja hafla ya kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwao.

Wamejumuika pamoja na wazazi wao, dada na kaka zao, ndugu, jamaa na marafiki zao kwenye hafla hiyo iliyofanya sana na kushuhudiwa na jicho la BMG.
Kenny akimlisha keki baba yake mzazi
Kenny akimlisha keki mama yake mzazi
Kenny akimlisha keki baba yake mdogo
Kenny akimlisha keki dada yake
Wakamwana watarajiwa, pia wamejumuika kwenye hafla hiyo. Watoto ni wajukuu wa familia.
Watoto waliozaliwa wanapenda sana game ya soka, hivyo keki imetengenezwa kwa muundo wa game hiyo
Hizi ni keki mfano wa game pamoja na timu za mpira wanazopenda
Wanafamilia wakifurahia kwenye hafla hiyo
Wa kwanza kushoto ni rafiki wa vijana hao. Wengine ni wazazi wa vijana hao. Wazazi wamewahimiza vijana wao kuuendeleza upendo huo ili udumu miaka yote kwani hiyo ni hatua nzuri ya kuyafikia mafanikio yao maishani ikiwa watashirikiana pamoja.

No comments:

Powered by Blogger.