LIVE STREAM ADS

Header Ads

WITO WA RC MAKONDA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory
Wito umetolewa kwa watumiaji wa huduma ya maji mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wanalipi kwa wakati ankara zao za maji  sambamba na kulinda miundombinu ya maji ili kuifanya huduma ya upatikanaji wa maji safi kuwa endelevu mkoani humo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam PAUL MAKONDA alipokuwa akitoa taarifa juu ya maadhimisho ya wiki ya maji kimataifa katika mkoa huo ambayo huadhimishwa duniani kote machi 16 hadi 22 kila mwaka.

Makonda ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu serikali ya mkoa wa Dar es salaam imelenga kuhamasisha na kuwaelimisha wananchi ,viongozi wa serikali za mitaa pamoja na kamati za maji kuhusu namna bora ya usimamizi wa shughuli za maji katika maeneo yao na taratibu za umiliki wa visima pamoja kufanya usafi na upandaji wa miti katika maeneo ya vyanzo vya maji ikiwemo mitadi ya Mbagala na Pugu na miradi mingine 20 ambayo itakabidhiwa rasmi kwa shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam (DAWASCO).

Akiyataja mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa Huduma ya maji katika mkoa wa Dar es salam katika kipindi cha mwezi machi 2016 hadi machi 2017 MAKONDA amesema kuwa kukamilika kwa mradi mkubwa wa ruvu chini ambai umeongeza upatikanaji wa maji kutoka lita milionj 182 kwa siku mpaka kufikia lita milioni 270  kwa siku sambamba na kukamilika kwa visima 15 kati ya 20 vya kimbiji na mpera ambavyo vitaongeza upatikanaji wa maji kwa lita milion 260 ifikapo mwaka 2019/2020.

No comments:

Powered by Blogger.