LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATENDAJI DAWASCO WATAKIWA KUONGEZA NGUVU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory
Wito umetolewa kwa Watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi Jijini Dar es salaam (DAWASCO), kuongeza nguvu katika usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi kuliko kuwekeza katika uzalishaji kama ilivyo sasa.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, alipotembelea ofisi za Dawasco na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo, ambapo amewataka kuongeza kasi katika usambazaji wa Maji na kuboresha miundombinu.

Aidha Profesa Mkumbo ametoa rai kwa Taasisi zisizolipia huduma hiyo kusitishiwa mara moja kama ambavyo Agizo la Rais Magufuli kwa wasiolipia huduma ya Umeme kusitishiwa huku akiwataka waanze kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji wa maji pamoja na vyanzo vyake ili kuzuia upotevu wa maj.

Awali akiwasilisha ripoti ya hali ya utoaji huduma wa Mamlaka hiyoMkurugenzi Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kwa sasa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani changamoto ya Huduma za maji safi zimepungua.

No comments:

Powered by Blogger.