LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAREHE RASMI YA KUANZA KWA MKUTANO WA KIMATAIFA WA OYES 2017 YAJULIKANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Tarehe rasmi ya kuanza kwa mkutano mkubwa wa kitaifa na kimataifa wa OYES (Open your Eyes and See) 2017 unaoandaliwa kila mwaka na kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza imejulikana.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amebainisha kwamba mkutano huo utaanza jumamosi Mei 27 na kufikia tamati jumapili Juni 04, 2017 katika viunga vya kanisa hilo vilivyopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza.

Kupitia BMG Habari, Dkt.Kulola amebainisha kwamba waimbaji na watumishi wa Mungu kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Mchungaji Garry White kutoka Amerika watahudumu katika mkutano huo.

Mafundisho pamoja na mahubiri ya neno la Mungu yaliyolenga kumfungua kila mmoja ili aone Ukuu wa Mungu yatafundishwa katika mkutano huo na kama ilivyo kawaida mamia ya wananchi wanatarajiwa kufunguliwa kwenye mkutano wa OYES 2017.

No comments:

Powered by Blogger.