LIVE STREAM ADS

Header Ads

Matumaini ya timu ya Pamba kucheza Ligi Kuu

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Binagi Media Group
Timu ya Soka ya Pamba imekubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Alliance kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza wa kuwania kucheza ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Licha ya matokeo hayo, bado timu hiyo inayo matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michezo yake ijayo ya mzunguko wa pili hususani katika michezo ya nyumbani na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kupanda ligi kuu.

Katika mchezo wa huo uliochezwa jana, mabao ya Alliance yalipachikwa na Shaban William na Dickson Abundo huku lile la Pamba likipachikwa kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Seveline Costantine.

Makocha wa timu hizo ambazo zote zinatokea Jijini Mwanza, wanazungumzia mchezo huo pamoja na mikakati ya kila timu katika katika kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo ijayo.

No comments:

Powered by Blogger.