WALICHOAGIZWA MADAKTARI HII LEO
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Dkt.Abisalam Omary ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za tiba na tathimini
WCF, amesema mfuko huo unawajengea uwezo madaktari hao ili kufanya tathmini
sahihi kwa wagonjwa wanaoumia kazini ama wasaidizi wao.
Na Binagi Media Group
Madaktari pamoja na Waganga nchini wametakiwa kutumia weledi wa
taaluma yao katika kuhudumia wagonjwa hususani wafanyakazi wanaoumia kazini kwa
kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati.
Mganga Mkuu mkoani Mwanza Dkt.Leonard Subby ameyasema hay oleo wakati
akifunga mafunzo ya siku tano kwa madaktari na waganga kutoka mikoa ya Kanda ya
Ziwa yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini WCF.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madaktari pamoja na Waganga
ili kutambua namna bora ya kufanya tathimini kwa mfanyakazi aliyeumia akiwa
kazini.
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi akifunga mafunzo hayo hii leo
Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza akifunga mafunzo hayo yaliyoanza jumatatu wiki hii
Mgeni Rasmi, Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt.Leonard Subi akikabidhi vyeti vya ushiriki kwa madaktari walioshiriki mafunzo/ semina hiyo
Bonyeza HAPA kusoma zaidi
No comments: