LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meya wa Jiji la Mwanza akutana na Rais Magufuli

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Siku moja baada ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza kwenye mapokezi ya Rais Dkt.John Magufuli, hatimaye jana alikutana na Rais Magufuli alipokuwa akizindua kiwanda cha Victoria Polybags & Moulders kilichopo Igogo!

Na Binagi Media Group
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa kiwanda cha vifungasgio Igogo
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akiwasilisha salamu zake kwenye uzinduzi huo
Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Dkt.Charles Mwijage akizungumza kwenye uzinduzi huo na kubainisha kwamba serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuhakikisha nchi inakuwa na viwanda vingi
Mkurugenzi wa kiwanda cha Victoria Polybags & Moulders akizungumza kwenye uzinduzi wa kiwanda hicho
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo akiwasilisha salamu zake
Diwani wa Kata Igogo Jijini Mwanza akionyesha fedha shilingi Milioni tatu alizopokea kutoka kwa Rais Magufuli ili kuboresha shule mbili za sekondari zilizo katika Kata hiyo
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Igogo, Justine Sagara (kulia) pamoja na viongozi wengine wa Kata hiyo wakifurahia baada ya kupokea shilingi Milioni Moja kutoka kwa Rais Magufuli kwa ajili ya shughuli za ofisi hiyo
Rais Magufuli akizindua kiwanda cha Victoria Polybags & Moulders
Bonyeza HAPA kwa habari zaidi

No comments:

Powered by Blogger.