Waziri wa Nishati azindua mradi wa REA Manispaa ya Ilemela
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith
Ferdinand, BMG
Waziri wa
Nishati Mhe.Medard Kalemani serikali itaendelea kusambaza huduma ya umeme kote
nchini ili kuwawezesha wananchi kutumia huduma hiyo kujiletea maendeleo.
Mhe.Kalemani
ametoa kauli hiyo wakati akizundua mradi wa umeme REA awamu ya tatu katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Aidha
aliagiza shirika la umeme nchini TANESCO kuhakikisha inatekeleza kwa wakati
zoezi la uunganishaji umeme katika Mitaa ya Lugashi, Bugando na Kabusungu na
kwamba zoezi hilo lisimwache mwananchi hata mmoja.
Naye mbunge
wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi alisema asilimia kubwa ya wakazi wa jimbo hilo wanahitaji huduma ya
umeme kwani wengi wao bado hawajafikiwa na huduma hiyo.
Mmoja wa
wakazi wa Manispaa ya Ilemela, Deus Siyantemi alifurahi kufikiwa na huduma ya
umeme na kubainisha kwamba itawasaidia kuanzisha miradi ya maendeleo ikiwemo
mashine za kusaga na kukoboa nafaka.
No comments: