Alliance watamba michezo ijayo Ligi Kuu Tanzania Bara
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Timu ya
Alliance FC imetamba kujipanga vyema kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Azam FC
utakatimua vumbi kesho Septemba 23,2018 katika uwanja wa CCM kirumba.
Mkuu wa
Idara ya Habari na Mawasiliano ya timu hiyo, Jackson Mwafilango anasema baada
ya kupoteza michezo minne na kutoka sare moja wanaendelea kukiimarisha kikosi
chao na wanaimani katika mchezo wao na Azam FC wanaweza kuibuka na ushindi.
Mwafilango
amesema benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mbwana Makata wanaimani na
wachezaji wao, na kadri mechi zinavyopita ndivyo wanavyozidi kuimarika na
kujifunza mbinu mpya.
"Kikosi
chetu baada ya kuwa ugenini takribani wiki tatu kimejifunza mambo mengi ikiwemo
mbinu mpya, ambapo katika mchezo wetu na Azam FC tunaweza kuibuka na ushindi
mnaweza kushangazwa na mende kuangusha kabati na thamani ya cherehani
anaifahamu fundi wakati akichomeka uzi kwenye sindano, hivyo na sisi tunafahamu
umuhimu wa wachezaji wetu na tunaimani nao," alisema Mwafilango.
Amesema
yaliyopita yamepita japo wanaumia kupoteza michezo minne mfululizo hivyo
aliwaomba wanamwanza na mashabiki wa timu hiyo kwa ujumla kuendelea kuiunga
mkono kwani wapo imara na anaimani siku za kucheka zinakaribia.
Katika
mchezo huo timu ya Alliance FC itakuwa mwenyeji huku kiingilio kikiwa shilingi 5,000 jukwaa kuu na mzunguko 3,000 hivyo mashabiki
wamehimizwa kujitokeze kwa wingi ili kuwapa hamasa wachezaji.
No comments: