LIVE STREAM ADS

Header Ads

Balozi Mahiga aeleza namna bora ya kuadhimisha Sherehe za Uhuru

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augustine (wa kwanza kulia) pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakikata keki kwenye hafla ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augustine Mahiga akizungumza kwenye hafla ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akizungumza mele ya Wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Mtangazaji wa KTN, Mark Masai akitoa historia fupi jinsi nchi ya Kenya ilivyopata uhuru wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.


Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema kuwa wakati wa kuadhimisha Uhuru ni lazima kuwakumbuka viongozi waliopigania Uhuru huo.

Mahiga aliyasema hayo jana wakati sherehe za Uhuru wa Nchi ya Kenya kwa wakenya waishio Tanzania iliyofanyika katika ukumbi Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa Kenya inaadhimisha miaka 55 ni kutokana na Baba wa Taifa wa nchi hiyo Jomo Kenyatta kupigana mpaka kupatikana kwa Uhuru ambao wa Kenya wanaendelea kuwa wamoja mpaka sasa. 

Mahiga alisema Tanzania na Kenya zina uhusiano ambao ulitokana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo mafanikio hayo ndio nchi mbili zinaendelea kufaidi. 

Aidha alisema miaka 55 ni mingi kwa Kenya kuendelea kulinda misingi iliyoachwa na viongozi waliopigania Uhuru.

Nae Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu alisema kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa na historia na kufanya wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uchumi unaotegemeana katika biashara pamoja na Uwekezaji.

Alisema kuwa Tanzania zimefungua Milango ya biashara kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya kuwa na nia njema kurahisisha biashara pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, akisisitiza kwamba Kenya imefungua milango kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya Uwekezaji pamoja na biashara bila vikwazo vyovyote. 

Katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya, viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao.

No comments:

Powered by Blogger.