LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita yapokea vifaa tiba kutoka APHFTA

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Mkurugenzi wa Miradi taasisi ya APHFTA, Elizabeth Bonareri (kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (kulia) printa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. Mashine hiyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyotolewa na taasisi ya APHFTA kuboresha huduma hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa Miradi taasisi ya APHFTA, Elizabeth Bonareri (kushoto), akimkabidhi Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (kulia) printa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. Mashine hiyo ni miongoni mwa vifaa tiba vilivyotolewa na taasisi ya APHFTA kuboresha huduma hospitalini hapo.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (kulia), akimkabidhi Mratibu wa Malaria mkoani Geita, Dkt. Moses Simon (kushoto) vifaa tiba vilivyotolewa na taasisi ya APHFTA kwa ajili ya kusaidia upimaji Malaria katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita.
Mkurugenzi wa Miradi taasisi ya APHFTA, Elizabeth Bonareri (kushoto), akifafanua jambo kuhusu vifaa tiba vilivyotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa Malaria katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita. Wengine ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (katikati) pamoja na Mratibu wa Malaria mkoani Geita, Dkt. Moses Simon (kulia).
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu (katikati) akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel (hayuko pichani) baada ya kupokea vifaa tiba kutoka taasisi ya APHFTA.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Geita, Herman Matemu akifungua kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya Malaria mkoani Geita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. Kikao hicho kiliandaliwa na taasisi ya APHFTA na kuambatana na zoezi la kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia upimaji Malaria katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita.
Mratibu wa Afya kutoka taasisi ya APHFTA, Dr.Berezy Makaranga akiwasilisha tathmini kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo kutoka taasisi ya Afya MicroFinance Limited, Phares Kapinga akifafanua namna taasisi hiyo inavyowasaidia mikopo watoa huduma za afya ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mchango wake kuhusu mapambano dhidi ya Malaria ambapo aliwasihi wadau wa mapambano dhidi ya Malaria mkoani Geita kuendelea kuweka mipango thabiti juu ya namna bora ya kupambana na ugonjwa huo.
Wadau wa mapambano dhidi ya Malaria mkoani Geita wakifuatilia kikao hicho.
Kikao cha tathimini baina ya wadau wa mapambano ya Malaria mkoani Geita kikiendelea.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Chama cha Watoa Huduma za Afya Binafsi Tanzania (APHFTA), kimekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Milioni 19 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Geita lengo likiwa ni kuboresha huduma ya upimaji Malaria kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Miradi APHFTA, Elizabeth Bonareri alisema vifaa hivyo ni pamoja na "Microscope" na kwamba chama hicho pia kimetenga Tsh. Milioni 30 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa jengo la maabara ya Hospitali hiyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Katibu Tawala Msaidizi, Herman Matemu alisema vifaa hivyo vitasaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi na hivyo kuomba vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

Mganga Mkuu mkoani Geita, Dkt. Japhet Simeo alibainisha kwamba juhudi mbalimbali ikiwemo kunyunyizia dawa ya ukoko majumbani, elimu sahihi kuhusu matumizi ya vyandarua vyenye dawa, utunzaji mazingira/ kufyekya nyasi na kufukia madimbwi pamoja na kuwahimiza wananchi kuwahi katika vipimo zimekuwa zikifanyika katika kupambana na ugonjwa wa Malaria ambapo pia ameishukru taasisi ya APHFTA kwa namna inavyoshirikiana na Serikali kupambana na ugonjwa huo.

Taasisi ya APHFTA kwa kushirikiana na kampuni ya Afya Micro-Finance kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo "Comic Relief" inatekeleza mradi wa kupambana na Malaria mkoani Geita ambapo juhudi hizo zimesaidia kiwango cha maambukizi kupungua kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 17 mwaka 2017/18.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.