LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAKUKURU mkoani Mwanza yajipanga kudhibiti mianya ya rushwa kwenye miradi ya maendeleo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza, Emmanuel Stenga, akizungumza na waandishi wa habari hii leo Januari 22, 2019 kuhusu utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kuanzia mwezi Oktoba hadi mwezi Disemba mwaka 2018.

Stenga amesema katika kipindi hicho, TAKUKURU mkoani Mwanza imefanya ukaguzi wa miradi 26 yenye thamani ya shilingi bilioni 31.6 ambapo miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Afya Igoma Jijini Mwanza (Tsh. Milioni 400), ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu Manispaa ya Ilemela (Tsh. Bilioni 18.8), uboreshaji Kituo cha Afya Malya na Mwamashimba wilayani Kwimba (kila kimoja Tsh. Milioni 400), ujenzi miundo mbinu katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukerewe (Tsh. Milioni 400), ujenzi Chuo cha Ualimu Murutungu Ukerewe (Tsh. Bilioni 1.5), ujenzi Kituo cha Afya Koromije wilayani Misungwi (Tsh. Milioni 500).

Amesema lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana kwa kila mradi huku miradi yote ikitekelezwa kwa ubora uliokusudiwa pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa katika miradi hiyo ili kuokoa fedha za Serikali na za wafadhili zisifanye ubadhilifu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.