LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko awapa somo wananchi kuelekea Uchaguzi Mdogo 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Madini amewaasa wananchi kujiandaa kushiriki Uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa Novemba 24, 2019 kwa kuwachagua viongozi sahihi watakaohamasisha maendeleo.

Biteko alitoa rai hiyo Septemba 19, 2019 wakati akizungumza na wananchi katika Kata ya Namonge jimboni humo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utekelezaji wa shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo.


Katika kuunga mkono juhudi za wananchi kimaendeleo, Biteko alichangia mifuko 358 ya simenti, mabati 20 pamoja na matofali 500 kama alivyoombwa na wananchi ili kusaidia ukamilishaji wa Zahanati ya Namonge, choo cha Zahanati hiyo pamoja na choo cha Shule ya Msingi Namonge.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.