Maonesho ya Madini Geita "NHIF watoa huduma bure kwa wananchi"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki Maonesho ya
pili ya Teknolojia na Uwekezaji katika Madini yanayofanyika mkoani Geita
kuanzia Septemba 22-29, 2019.
Meneja wa
NHIF Mkoa Geita, Elias Odiambo amewahimiza wananchi wanaofika kwenye maonesho
hayo kutembelea banda la mfuko huo ili kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo
huduma ya vipimo bure kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Odiambo
ametoa rai hiyo Septemba 23, 2019 baada ya waandishi wa habari kutembelea banda
la NHIF ili kujifunza huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo na kuongeza
kwamba tayari zaidi ya wananchi 300 wamehudumiwa kwenye banda hilo.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: