LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella aongoza kikao cha wadau wa kilimo, mifugo na uvuvi mkoani Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Septemba 17, 2019 amefungua na kuongoza kikao cha wadau wa kilimo, mifugo na uvuvi mkoani Mwanza, kilichoratibiwa na taasisi ya ushauri wa miradi ya maendeleo DABERG.

Mongella alitumia kikao hicho kutoa rai kwa viongozi pamoja na wadau hao kutoka na azimio la mambo matatu muhimu kwenye kila sekta (kilimo, mifugo na uvuvi) ili kuyatekeleza ipasavyo na kutoa mrejesho kwenye kikao kijacho mwezi Novemba mwaka huu 2019.

Katika kikao hicho, taasisi ya DABERG pia ilitoa mrejesho wa utekelezaji mradi wa mapinduzi ya kilimo mkoani Mwanza kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kuonesha kwamba umeleta tija katika kufufua miradi mbalimbali ya kilimo iliyokuwa imekufa huku matarajio yakiwa ni kushirikisha zaidi wadau wa sekta binafsi ili kuendeleza shughuli za mradi huo pindi utakapofikia tamati.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.