LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mongella atembelea Kituo cha kutengeneza viungo bandia vya binadamu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Septemba 18, 2019 ametembelea Kituo cha kutengeneza viungo bandia vya binadamu (Mwanza Prosthetics & Orthotics Workshop) na kuvutiwa na huduma zinazotolewa kituoni hapo.

Kituo hicho kilichopo Pasiansi Manispaa ya Ilemela kinatengeneza viungo mbalimbali bandia kwa watu wenye ulamavu ikiwemo miguu pamoja na kurekebisha ulemavu wa viungo mbalimbali mwilini.

Mongella amechangia mafuta lita 200 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Kituo hicho kufikisha huduma tembezi (Mobile Workshop) huku pia akitoa ahadi ya kumpatia mtaji wa kuanzisha mradi wa saluni binti AsianPatrick ambaye amenufaika na viungo bandia kituoni hapo ambaye kwa sasa anasoma chuo cha urembo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.