Binti aliyepoteza miguu, vidole vya mikono na kizazi ashangaza wengi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Binti Asia
Patrick mkazi wa Bwiru Wilaya Ilemela mkoani Mwanza aliyepoteza miguu, vidole
tisa vya mikono pamoja na kizazi kutokana na matatizo ya uzazi, ameonesha
matumaini makubwa ya kutimiza na ndoto zake maishani baada ya kupata viungo bandia.
Ni baada ya
binti huyo kuwa mmoja kati ya wa wanufaika wa Kituo cha kutengeneza viungo
bandia vya binadamu cha Mwanza Prosthetics & Orthotics Workshop kilichopo
Pasiansi wilayani wilayani Ilemela.
Septemba 18,
2019 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella alitembelea Kituo hicho na kukutana na
binti Asia ambapo alifurahishwa na ucheshi wake licha ya hali aliyonayo na
kuahidi kumuongezea mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara ya saloni pindi
atakapohitimu mafunzo yake ya urembo.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: