MISUNGWI CDTTI, TAESA WAWAPIGA MSASA WANAFUNZI
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Ajira na Kazi Tanzania (TAESA), kimewajengea uelewa wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali ikiwemo ajira za mikataba, huduma za kazi na mahusiano bora kazini.
Hayo yamejiri wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa chuo hicho na kuhudhuriwa na wanafunzi pamoja na watumishi.
Watumishi wa Misungwi CDTTI na TAESA waliwasilisha mada muhimu kuhusu nidhamu, maadili, uwajibikaji na kuheshimu taratibu za kazi.
Pia mawasiliano bora, uongozi na ubunifu mahala pa kazi, wakisisitiza namna ya kujenga mahusiano chanya na kuongeza tija katika mazingira ya kazi.
Aidha kikao hicho kilieleza wajibu wa TAESA kwa wanafunzi pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo, ikiwemo kuwajengea uwezo wa kielimu, uongozi na maadili ili kuwaandaa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na taifa.










No comments: