Mila potofu ya “samba” yazidi kulalamikiwa wilayani Kishapu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mila potofu
ya “samba” inayohusisha baadhi ya wazazi na walezi kuwapeleka mabinti zao kwa
waganga wa kienyeji kuchanjwa dawa ya kuvutia wanaume, imeendelea kulalamikiwa
kwa kuchochea mimba na ndoa za utotoni katika Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.
Hayo yalielezwa
Oktoba 02, 2019 kwenye kampeni ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake
na watoto iliyofanyika Kata ya Uchunga, inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya
Kishapu kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI.
Katika
kipindi cha mwaka kwa mwaka 2017/19 kesi 101 za wanafunzi kubeba ujauzito ziliripotiwa
polisi wilayani Kishapu hivyo licha ya elimu inayoendelea kutolewa, bado mamlaka
za Serikali zimetakiwa kuchukua hatua ili kupambana na mila hiyo potofu.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini
No comments: