LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau waadhimisha Siku ya Wazee Duniani katika Kituo cha Busanda Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wadau wa maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko wamesherehekea Siku ya Wazee Duniani 2019 kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Milioni 2.5 kwa ajili ya wazee wanaoishi katika Kituo cha Busanda kilichopo Kata ya Usanda, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Wadau hao walifika katika Kituo hicho Jumamosi Oktoba 5,2019 kusherehekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba Mosi.

Akizungumza katika Kituo hicho kinachohudumia Kaya 20 za wazee, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta alisema wameamua kusherekea siku ya wazee duniani katika Kituo hicho kwa kuwapatia mahitaji muhimu yanayotakiwa ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili wazee hao.

Mboneko alivitaja vitu vilivyotolewa na wadau kuwa ni magodoro 20, shuka 40, vyandarua 20, mchele kilo 200, sukari kilo 50, unga wa sembe kilo 225, maharage kilo 20, sabuni za miche boksi moja, sabuni ya unga kilo 15, mafuta ya kupaka katoni mbili, mafuta ya kupikia lita 20, dagaa debe mbili, dawa za meno katoni mbili, viberiti katoni mbili, chumvi katoni moja, juisi katoni mbilipamoja na nyanya debe moja. 

Mkuu huyo wa Wilaya aliwashukuru wadau waliojitokeza kutoa msaada wa vitu hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni 2.5 ambao ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll, Seif Said Seif aliyetoa msaada wa magodoro 20, vyandarua na shuka vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na laki nne.

"Kwa namna ya pekee niwashukuru wadau walioguswa kutoa mchango kusaidia wazee wetu hawa. Wadau hawa ni pamoja Mkurugenzi wa Makampuni ya Superdoll, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Azza Hilal, Watumishi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba na watumishi wa benki ya NBC" alisema Mboneko. 

"Wadau wengine ni Kwaya ya Malaika Wakuu Kanisa Katoliki Ngokolo, Familia ya Richard Male, Familia ya mama Shine, Mama Mihambo na marafiki zake, Gilitu, Said Makilagi (Musoma Food), Dada Scola na Lightness, waandishi wa habari na wadau wengine ambao sijawataja ambao kwa pamoja wamefanikisha kupatikana kwa mahitaji haya kwa ajili ya wazee wetu" aliongeza Mboneko. 

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad aliahidi kuwalipia Bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) wazee 11 waliopo katika Kituo cha Busanda ili wapate huduma za afya bila usumbufu. 

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa Serikali za Vijiji na Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 kwa kujitokeza kugombea na kuchagua viongozi wenye kusaidia jamii. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika Kituo cha kulelea wazee cha Busanda.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akielezea kuhusu msaada uliotplewa katika Kituo cha wazee Busanda.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kituo cha Kulelea Wazee cha Busanda, Elias Shilanga akielezea kuhusu kituo hicho.
Mahitaji mbalibali yaliyotolewa na wadau.
Wadau wakijiandaa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wazee katika Kituo cha Busanda. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akikabidhi unga wa sembe Mary Barabara katika Kituo cha kulelea Wazee cha Busanda ambapo kila mzee alipokea msaada wa unga wa sembe, mchele, sukari, mafuta ya kupaka, mafuta ya kupikia, sabuni, godoro, shuka mbili, vyandarua, maharage nk.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (kushoto) akikabidhi godoro, shuka, chandarua kwa mmoja wa akina bibi wanaoishi katika Kituo hicho.
Zoezi la kukabidhi godoro, shuka na chandarua likiendelea. 
Bibi akifurahia baada ya kupokea mahitaji mbalimbali.
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog, Kadama Malunde ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga akisaidiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kubeba mfuko wa nyanya wakati wa kugawa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya wazee katika Kituo cha Busanda.
Zoezi la kuweka sabuni ya unga kwenye mifuko likiendelea. 
Mdau Said Nassoro akigawa sabuni ya unga. 
Mzee Zacharia Makaranga akiwashukuru wadau waliotoa msaada kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha Busanda.
Bibi akishukru kwa msaada uliotolewa na wadau.
Imeandaliwa na Kadama Malunde pamoja na Marco Maduhu - Malunde 1 Blog

No comments:

Powered by Blogger.