LIVE STREAM ADS

Header Ads

AMAIZING “wafanyakazi benki ya CRDB Mwanza washerehekea mwaka 2020”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB kutoka matawi yote mkoani Mwanza wameuanza mwaka 2020 kwa kuandaa hafla ya pamoja iliyofanyika Januani 25, 2020 katika fukwe za Capri Kabana jijini Mwanza.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitaa alisema hafla hiyo itaongeza ari kwa wafanyakazi katika kutoa huduma bora mwaka huu 2020 huku pia ikiwajengea mtandao mpana wa kufahamiana miongoni mwao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa benki ya RCDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umoja (tema work) miongoni mwa wafanyakazi wa benki hiyo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB Mkoa Mwanza wakimsikiliza Meneja wa benki hiyo Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa benki ya RCDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta (kushoto) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya CRDB Makao Makuu akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya CRDB jijini Mwanza ambaye pia alisherehesha vyema hafla hiyo.
 Endelea kutazama picha zaidi kuhusiana na hafla hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.